Teknolojia imekua kwa kiasi kikubwa kwa sasa na kurahisisha shughuli zote zilizokua zikifanywa na binadamu kwa kubadili, kuboresha na pia kuzifanya kwa haraka Zaidi. Kuanzia katikati ya miaka ya 2010s kumekua na ongezeko kubwa la ukuaji wa teknolojia duniani hasa matumizi ya Akili Bandia au Artificial Intelligence (AI) katika utendaji wa shughuli nyingi zilizokua zikifanywa na binadamu kuanza kufanya kirahisi na computer. Hivyo, kwasasa Akili Bandia AI inaweza kuandaa Makala mbalimbali, kuchakata kiasi kikubwa cha data, kudesign mifumo n ahata kufanya shughuli zilizokua zinahitaji ubunifu wa kibinadamu kama kuchora, kuandika code za program, kutengeneza videos nakadhalika,
Kutokana na maendeleo haya, leo ningependa kukuelewesha ujuzi muhimu sana sokoni kwasasa kwa upande wa designing yaani Kuedit picha. Picha hueditiwa kwa ajili ya matumizi ya kila siku kama vile kuweka muonekano mzuri wa picha za matukio, kutumia kwenye matumizi ya mtandaoni na kijamii, kutengeneza passiport na kuweka mazingira bunifu ya kuvutia.
Katika Makala hii tutaangalia namna ya kuifanya picha yako ambayo ina muonekano hafifu au imepigwa mahali penye mwanga mdogo ili iweze kuwa na ubora na muonekano wa kisasa kwa kutumia Akili Bandia ya ChatGPT kupitia muongo mdogo tu wa kuipatia maneno maalumu tunaita (Prompt). Fuata hatua hizi hapa kuendelea….
HATUA YA KWANZA. Ingia kwenye store ya Playstore au Appstore na udownload application ya Chat GPT kama unatumia simu janja (smartphone) au ingia kwenye browser yako mf. Chrome na uandike https://chatgpt.com kisha ingia kwenye website kama unatumia computer au laptop.
HATUA YA PILI. Hatua hii unapaswa kulog in kwenye akaunti yako ya Chat GPT kama ulikua nayo tayari au fungua akaunti mpya kwa kuchagua Sign Up na kisha kujaza taarifa zako muhimu kadri ulivoulizwa. Au unaweza kusign Up kwa hatara Zaidi ukulog in kwa kutumia email iliyopo tayari kwenye simu na kuruhusu Chat GPT iweze kuungana na email moja kwa moja.
HATUA YA TATU. Baada ya kumaliza kulog in/ kusign up akaunti sasa utakua ndani ya uwanja wa kuchat moja kwa moja na Chat GPT. Bonyeza alama ya msalaba na chagua Photos kicha utapelekwa moja kwa moja kwenye files zako au folder chagua picha unayotaka kuifanyia kazi na kicha iruhusu ili urudi kwenye uwanja wa kuchat.
HATUA YA NNE. Baada ya picha kumaliza kuupload kabla ya kutuma meseji andika maneno haya kuambatana na hiyo picha “NAHITAJI PICHA YANGU IWE NA MUONEKANO MZURI WA KISASA NA ING’AE” kisha tuma ujumbe kwa Chat GPT.
Hongera! Mpaka hapa utakua umefanikiwa na umemaliza kazi yako. Subiri Chat GPT ifanye kazi yake ndani ya muda mchache picha yako itarudi ikiwa na muonekano mzuri Zaidi ya uliyoiweka na utaweza sasa itumia kwa matumizi binafsi au hata kwenda kuisafisha bila tatizo.
NB: ikumbukwe kuwa Chat GPT ni programu ya kisasa inayotumia teknolojia ya Akili Bandia au AI kuchakata data mbalimbali kwa haraka hivyo kurahisisha utendaji kazi wa maisha yetu ya kila siku. Tafadhali, tuambie kwenye comment ni jambo gani Zaidi ungependa kujua uweze kulifanya kwa kutumia program hii ya Chat GPT na tutaandaa Makala yake punde.
Comments
Post a Comment