JINSI YA KUTAZAMA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2026 MTANDAONI; MUONGOZO KAMILI KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI
Matokeo ya Kidato cha Pili ni hatua muhimu sana katika maisha ya mwanafunzi wa sekondari Tanzania. Matokeo haya yanatoa taarifa kuhusu ufanisi wa mwanafunzi baada ya kumaliza mwaka wa pili wa masomo, na ni muhimu kwa hatua zinazofuata kama kujiandaa kwa kidato cha tatu au mikakati ya kuboresha ufaulu katika masomo mbalimbali. Matokeo haya yanatolewa rasmi na National Examinations Council of Tanzania (NECTA) kupitia njia mbalimbali, ikiwemo mtandao.
NECTA ni Nini? Na Kwa Nini Matokeo ya Kidato Cha Pili ni Muhimu?
NECTA ni chombo kinachosimamia mitihani ya kitaifa Tanzania, ikijumuisha mitihani ya darasa la saba, kidato cha pili, kidato cha nne, kidato cha sita na mingineyo. Matokeo ya Kidato cha Pili (inayojulikana kama Form Two National Assessment – FTNA) hutolewa kila mwaka baada ya mtihani kufanyika mwishoni mwa mwaka wa masomo. Matokeo haya ni muhimu kwa sababu: Huonyesha mahali mwanafunzi amesimama kitaaluma baada ya miaka miwili ya sekondari, husaidia watahiniwa, wazazi na walimu kupanga mikakati ya mafanikio ya masomo na pia ni kigezo muhimu kabla ya kuendelea na kidato cha tatu.
JINSI YA KUTAZAMA MATOKEO MTANDAONI
Matokeo ya kidato cha pili (FTNA) 2026 yanapatikana katika tovuti maalumu ya NECTA ambayo inasimamia na kuhifadhi matokeo ya darasa la pili, darasa la nne, darasa la saba, kidato cha kwanza, kidato cha pili, kidato cha nne, kidato cha sita na matokeo ya ualimu. Kutazama matokeo fuata hatua zifuatazo;
1. Fungua kivinjari (Browser) chako kwenye simu au computer na kisha tembelea tovuti hii (https://matokeo.necta.go.tz/)
2. Shuka chini na uchague MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA YA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2025
3. Hapa itatokeo orodha ya shule zote zilizofanya mtihani wa kitado cha pili mwaka 2025, hivyo unapaswa kufahamu namba au jina halisi la shule unayotaka kuangalia matokeo. Kwa muongozo wa haraka gusa dot tatu juu kulia mwa kivinjari chako na chagua Find in Page na kisha andika namba au jina la shule unayoitaka kuweza kutafuta kwa haraka zaidi. Mf.S239 kwa St. Francis Girl's Sec
4. Baada ya kucheza na orodha ya shule, utaona orodha ya wanafunzi pamoja na majina yao, nambari za mtihani (index numbers) na alama za kila somo. Hii ina maana unaweza sasa kuona matokeo yako kwa undani na mambo mengine kama ufaulu wa shule, kila somo na nafasi ya shule kitaifa kwenye kategozi yake.
Kupata matokeo ya Kidato cha Pili kupitia tovuti ya NECTA ni mchakato wa hatua kwa hatua ambao unaweza kufanyika kirahisi endapo unafuata mwongozo sahihi. Mfumo huu wa mtandaoni unawawezesha watahiniwa, wazazi, na walimu kupata matokeo kwa haraka, kwa usahihi na kwa wakati muafaka bila hitaji la kusafiri kwenda ofisi za shule au NECTA. Matokeo haya ni chachu ya mipango ya masomo na hatua za baadaye za elimu.





Comments
Post a Comment