Afrika imeendelea kuwa kitovu cha vipaji vya sanaa ya
uigizaji, na miaka ya hivi karibuni imeshuhudia kuibuka kwa wasanii wa filamu
waliotamba ndani na nje ya bara. Wasanii hawa wamechangia pakubwa kukuza tasnia
ya filamu barani Afrika kwa ufanisi mkubwa, wakileta simulizi za Kiafrika
kwenye jukwaa la kimataifa. Hapa chini tunawaletea baadhi ya wasanii wa filamu
waliofanya vizuri zaidi Afrika kwa kuzingatia mafanikio yao kitaifa na
kimataifa, tuzo walizoshinda, na mchango wao katika tasnia.
1.
GENEVIEVE NNAJI (NIGERIA)
Genevieve ni mmoja wa waigizaji mashuhuri barani Afrika.
Alianza kazi yake katika tasnia ya filamu ya Nollywood akiwa na umri mdogo
sana. Filamu yake ya Lionheart (2018) ilifanya historia kwa kuwa
filamu ya kwanza ya Nigeria kununuliwa na Netflix. Pia amepata tuzo mbalimbali
kama Africa Movie Academy Award (AMAA)
na City People Entertainment Award. Baadhi
ya Movie zingine alizofanya ni kama; 30 Days (2006), Winds of Glory (2007),
Beautiful Soul (2008), Mirror Boy (2010), Doctor bello (2013) na Road to
Yesterday (2015).
2.
LUPITA NYONG’O (KENYA)
Lupita alizaliwa nchini Mexico lakini ana asili ya Kenya.
Mafanikio yake makubwa yalikuja kupitia filamu ya 12 Years a Slave (2013), ambayo ilimletea tuzo ya Oscar kama Muigizaji Bora Msaidizi. Ameigiza
katika filamu kubwa kama Black Panther,
Us, na Queen of Katwe, A Quiet place: Day One and The Jungle Book.
Anajulikana duniani kote kwa ufanisi wake wa hali ya juu katika kuigiza na kutetea
haki za wanawake na watu weusi.
3.
RAMSEY NOUAH (NIGERIA)
Ramsey ni mmoja wa waigizaji wakongwe na wanaoheshimika
sana katika kiwanda cha Nollywood. Ametambulika kwa uigizaji wake bora katika
filamu kama The Figurine, 30 Days in Atlanta, na Living in Bondage: Breaking Free. Pia
ameanza kuingia katika upande wa uongozaji wa filamu.
4.
CHARLIZE THERON (AFRIKA KUSINI)
Ingawa Charlize anafanya kazi zaidi Hollywood, yeye ni
mzaliwa wa Afrika Kusini. Alishinda tuzo ya Oscar kupitia filamu Monster (2003) na ameigiza filamu
nyingi maarufu kama Mad Max: Fury Road, Atomic
Blonde, Monster, The Old Guard and The Italian Job. Anaiwakilisha Afrika
vizuri sana kimataifa.
5.
OMOTOLA JALADE EKEINDE (NIGERIA)
Anajulikana kama "Omosexy", Omotola ni mmoja wa
waigizaji wa Nollywood walioweka historia. Ameshiriki zaidi ya filamu 300, na
mwaka 2013 aliorodheshwa kwenye orodha ya watu 100 wenye ushawishi mkubwa
duniani na jarida la TIME. Amechangia pia katika masuala ya kijamii kupitia
kazi zake na kampeni mbalimbali. Baadhi ya filamu alizoigiza ni pamoja na Blood Sister, Alter Ego, Mortal Inheritance
and Lockdown.
6.
FLORENCE KASUMBA (UGANDA/UJERUMANI)
Kasumba ni msanii mwenye asili ya Uganda lakini anafanya
kazi zake Ujerumani na Hollywood. Anajulikana kwa kuigiza kama Ayo katika
filamu za Black Panther, Avengers: Infinity War na The Falcon and the Winter Soldier. Ana
sifa kubwa kwa uigizaji wa nguvu na mwonekano wake wa kipekee. Baadhi ya movie
nyingine alizoshiriki ni pamoja na Criminal:
Germany, Kitz, Spides and Mute.
7. RMD
– RICHARD MOFE-DAMIJO (NIGERIA)
RMD ni msanii mkongwe, mwanasiasa, na mmoja wa watu
walioweka msingi wa Nollywood. Amekuwa mfano kwa wasanii wengi chipukizi. Uwezo
wake wa kuigiza kwa weledi mkubwa umeendelea kumuweka juu kwa miongo kadhaa.
Baadhi ya Movie alizoshirikishwa ni pamoja na The Black Book, Shanty Town, Far from Home, The Wedding Party and
Castle & Castle.
8.
LELETI KHUMALO (AFRIKA KUSINI)
Leleti alijulikana sana kwa uigizaji wake katika filamu ya Sarafina! (1992), ambayo iliangazia
harakati za kupinga ubaguzi wa rangi Afrika Kusini. Ameendelea kushiriki katika
filamu na vipindi vya televisheni, akibeba ujumbe wa kijamii na kihistoria.
Baadhi ya filamu zingine alizoshiriki ni Yesterday,
Cry; The Beloved Country and Free State.
9.
MAJID MICHEL (GHANA)
Majid ni mmoja wa waigizaji maarufu kutoka Ghana,
anayejulikana kwa filamu za mapenzi na drama. Amekuwa akishirikiana sana na
Nollywood na kushinda tuzo mbalimbali zikiwemo Africa Movie Academy Awards. Baadhi ya movie alizoshiriki ni pamoja
na A Taste of Sin, Passion of the Soul,
Heart of Men, Somewhere in Africa, Crime to Christ and House of Gold.
10.
JACKIE APPIAH (GHANA)
Jackie ameibuka kuwa mmoja wa waigizaji wanawake
wanaopendwa sana kutika Afrika Magharibi. Ana umaarufu mkubwa kutokana na
mtindo wake wa kipekee wa kuigiza, na amepata tuzo nyingi zikiwemo Ghana Movie Awards na AMAA. Ameigiza baadhi ya movie kama Princess Tyra, A Taste of Sin, Passion of
the Soul, The Perfect Picture and Mummy’s Daughter.
Wasanii wa filamu Afrika wamefanikiwa kuvuka mipaka ya
kitaifa na kufika hatua za kimataifa kwa bidii, vipaji na ubunifu wao. Wengi
wao si tu waigizaji, bali pia ni waongozaji, waandishi na watetezi wa masuala
ya kijamii. Kwa sasa, tasnia ya filamu barani Afrika inaendelea kukua kwa kasi,
na wasanii hawa wamekuwa mfano wa kuigwa kwa kizazi kijacho.
Hawa ni baadhi tu ya wasanii walioikuza sana sanaa ya
maigizo na uhamasishaji kwa miongo kadhaa hapo nyuma. Makala iyajo nitakuletea
list ya wasanii wengine ambao pia mchango wao hauwezi sahaulika katika tasnia
hii ya maigizo na uhamasishaji duniani wakitokea bara la Africa.
Comments
Post a Comment