Skip to main content

NAMNA YA KUFAHAMU KITAMBULISHO CHAKO CHA NIDA KAMA KIMEKAMILIKA NA MAHALI PA KUKIPATA KUPITIA SIMU YAKO

 

Habari mpendwa msomaji wa Makala hii, kama umekua ukijiuliza ni namna gani unaweza kujua kama kitambulisho chako cha Taifa (NIDA) kiko tayari au la na je! Ni mahali gani unaweza kwenda kukichukua ili uanze kukitumia kwa matumizi ya kila siku basi uko mahala sahihi kwasababu nitakuelekeza hatua kwa hatua hadi utafanikiwa kukipata kwa kutumia computer au simu yako ya mkononi.

MAANA YA KITAMBULISHO CHA TAIFA

Kitambulisho cha Taifa ni nakala inayoelezea taarifa muhimu za raia wa Tanzania kama vile jina, mahali anapoishi, jinsia na umri wake. Vitambulisho hivi nchini Tanzania hutolewa na mamlaka husika ya vitambulisho vya Taifa au NIDA kwa ajili ya kumtambua kila raia wa hapa nchini kuwa ni mkazi wa kudumu, mkazi muhamiaji au mkimbizi.

NAMNA YA KUFAHAMU KITAMBULISHO CHAKO KAMA KIKO TAYARI NA WAPI UTAWEZA KUKIPATA

Katika Makala iliyopita tulieleza namna unaweza kufahamu namba yako ya kitambulishocha Taifa na sasa tunaenda kuangalia ni mahali gani unaweza kukipata kitambulisho chako bila gharama yoyote. Kabla ya kuanza unapaswa kuwa na vitu vifuatavyo ;

1.  Jina ulilotumia kujisajili yaani jina la mwanzo, jina la kati na jina la mwisho.

2.  Mahali ambapo ulienda kuandikisha taarifa zako za kitambulisho yaani Mkoa, Wilaya, Kata na Mtaa.

Baada ya kuwa unafahamu hivo vitu viwili sasa utachukua simu yako au computer na kuingia kwenye kivinjari chochote nashauri Zaidi utumie Google Chrome kwasababu ni rahisi na inauwezo wa kufungua kurasa nyinyi bila usumbufu.  Baada ya kufungua kivinjari chako sasa ingia tovuti ya mamlaka ya vitambulisho vya Taifa kwa kusearch au kuandika kubonya kiungo hiki https://nida.go.tz/   hapa moja kwa moja utatokea ukurasa wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa kama inavyoonekana hapa chini.


Baada ya ukurasa wa NIDA kufunguka angalia upande wa juu kulia na tafuta maneno yaliyoandikwa KITAMBULISHO CHA TAIFA na kisha bonyeza na uchague FAHAMU KITAMBULISHO KILIPO.



Kisha itatokea hapa… 


Baada ya hapo gusa mkoa ulipojiandikishia taarifa zako, kisha gusa wilaya na mwisho kabisa gusa kata / kijiji kama unavoelekezwa na mfumo. Baada ya kumaliza hatua hizo zote yatatokea majina ya watu mbalimbali waliojiandikisha kata hiyo na utafute jina lako kulingana na herufi yako ya mwanzo. Mf. Joshua utashuka hadi ilipoanzia herufi J.

Kumbuka; majina pekee utakayoyaona katika ukurasa wa mwisho ni ya wale ambao vitambulisho vyao vimekamilika kwa mfumo wa hardcopy tu (yaani vitambulisho vyao vimeshachapishwa) na kutumwa kwenye ofisi husika. Hii inamaanisha kama usipoliona jina lako na namba ya NIDA unayo basi fahamu ya kuwa kitambulisho chako bado hakijachapishwa kwa mfumo wa hardcopy. Pia kuwa makini katika uchaguzi wa kata maana watu wengi husahau mahali halisi walipojiandikisha hivyo unashauriwa kuangalia jina lako na kata za jirani laweza kuwa humo.

Aidha kama utapenda kuingia mwenyewe moja kwa moja kwenye tovuti ya vitambulisho vya Taifa kwa njia fupi ni rahisi sana bonyeza kiungo hiki (https://vitambulisho.nida.go.tz/) na kisha fuata hatua zote kama ilivyoelezwa hapo juu kujua kama kitambulisho chako kimetokaau lah.

TAFADHALI USISITE KUACHA COMMENT YAKO MAHALI POPOTE ULIPOKWAMA AU PATA CHANGAMOTO. 

Comments

Popular Posts

JINSI YA KUTAZAMA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2026 MTANDAONI; MUONGOZO KAMILI KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI

  Matokeo ya Kidato cha Pili ni hatua muhimu sana katika maisha ya mwanafunzi wa sekondari Tanzania. Matokeo haya yanatoa taarifa kuhusu ufanisi wa mwanafunzi baada ya kumaliza mwaka wa pili wa masomo, na ni muhimu kwa hatua zinazofuata kama kujiandaa kwa kidato cha tatu au mikakati ya kuboresha ufaulu katika masomo mbalimbali. Matokeo haya yanatolewa rasmi na National Examinations Council of Tanzania ( NECTA ) kupitia njia mbalimbali, ikiwemo mtandao.  NECTA ni Nini? Na Kwa Nini Matokeo ya Kidato Cha Pili ni Muhimu? NECTA ni chombo kinachosimamia mitihani ya kitaifa Tanzania, ikijumuisha mitihani ya darasa la saba, kidato cha pili, kidato cha nne, kidato cha sita na mingineyo. Matokeo ya Kidato cha Pili (inayojulikana kama Form Two National Assessment – FTNA ) hutolewa kila mwaka baada ya mtihani kufanyika mwishoni mwa mwaka wa masomo. Matokeo haya ni muhimu kwa sababu: Huonyesha mahali mwanafunzi amesimama kitaaluma baada ya miaka miwili ya sekondari, husaidia watahiniwa, ...

HIGHLIGHTS 4 - 1: ARSENAL YAIPA KIPIGO KIKALI ASTON VILLA NA KUBAKIA KILELENI EPL

🔴⚪ ARSENAL WATHIBITISHA UBABE DHIDI YA ASTON VILLA BAADA YA USHINDI MNONO WA 4–1 Tarehe : 30 Desemba 2025 Uwanja : Emirates Stadium Arsenal waliendelea kuonyesha dhamira yao ya kupigania mafanikio makubwa msimu huu baada ya kuichapa Aston Villa kwa mabao 4–1 katika mechi ya kusisimua iliyochezwa kwenye Uwanja wa Emirates . Ilikuwa ni mechi iliyojawa na kasi, ushindani mkubwa na burudani ya hali ya juu, huku Arsenal wakithibitisha kwa vitendo kuwa wako katika kiwango cha juu sana. 🕒 MWANZO WA MECHI : ARSENAL WANZA KWA KASI Mara tu baada ya kipenga cha kuanza kusikika, Arsenal waliingia kwa kasi kubwa wakitawala umiliki wa mpira na kuwabana Aston Villa katika eneo lao. Mfumo wa pasi fupi, presha ya juu ( high press ) na kusogea kwa pamoja kuliwapa Arsenal udhibiti wa mchezo mapema. Leandro Trossard , aliyekuwa akicheza upande wa kushoto, alianza kuwasumbua mabeki wa Villa kwa mbio za kasi, dribbling za kuvutia na kupandisha mashambulizi mara kwa mara. ⚽ GOLI LA KWANZA : ...

LIVERPOOL WAANZA MWAKA KWA SARE TASA: LEEDS UNITED WAWEKA KAMBI ANFIELD

UTANGULIZI Mwaka mpya wa 2026 umeanza kwa mtindo wa kipekee katika Ligi Kuu ya England, ambapo Liverpool na Leeds United walikutana Anfield na kuishia kwa sare tasa ya 0-0. Mashabiki wa Reds walitarajia kuona mwanzo wa kishindo chini ya kocha Arne Slot , lakini ukuta wa Leeds uliosimamiwa na Daniel Farke ulihakikisha hakuna mabao yaliyopatikana. Hii ilikuwa mechi ya kwanza ya mwaka na pia clean sheet ya kwanza kwa Leeds tangu Agosti, ikitoa taswira ya nidhamu na uimara wa kiulinzi dhidi ya moja ya timu kubwa zaidi nchini. Muhtasari wa Mechi - Tarehe na Mahali : 1 Januari 2026, Anfield   - Matokeo : Liverpool 0-0 Leeds United   - Kocha Liverpool : Arne Slot   - Kocha Leeds : Daniel Farke   Mambo Muhimu ya Mechi - Udhibiti wa mchezo: Liverpool walimiliki mpira kwa 69% lakini walishindwa kutengeneza nafasi safi za kufunga.   - XG (Expected Goals): Liverpool walitengeneza takribani 1.96xG, ikionyesha walikuwa na nafasi lakin...