UTANGULIZI
Namba ya NIDA (National Identification Number i.e.
NIN) ni namba ambayo anapewa raia wa nchi ya Tanzania baada ya kujiandikisha
kwenye serikali yake ikiwa kama utambuzi wa uraia wake nchini. Namba hii inapatikana
katika kitambulisho cha Taifa cha uraia kwa raia wote wa Tanzania na hutumika
katika shughuli mbalimbali za kijami na kiserikali ndani na nje ya nchi.
Ni muhimu kwa kila raia kuwa na kitambulisho cha
Taifa (NIDA), lakini kutokana na ugumu wa utengenezaji wa vitambulisho hivi
kumekua na uchelewaji wa utengenezaji wa nakala halisi ya kitambulisho na
kupelekea raia wengi kutumia tu namba zilizopo kwenye kitambulisho hicho kwa
kujisajili katika huduma mbalimbali pindi wanaposubiri nakala halisi ya vyeti
vyao.
Baadhi ya watu wamekuwa wakijiuliza ni namna gani
wanaweza kuipata namba hii bila ya kwenda ofisi ya serikali au mtaa
walipojiandikisha!. Bahati nzuri kutokana na mabadiliko ya kukua kwa sayansi na
teknolojia serikali kupitia wizara yake imetengeneza website ambayo
itamuwezesha raia yeyote kujipatia huduma anayotaka kuhusu kitambulisho chake
cha Taifa (NIDA) bila gharama yeyote ile iwapo atakua na kifaa chochote
kitakachomuwezesha kufanya ivo yani simu janja (smartphone) au computer. Baadhi
ya huduma hizo ni upataji wa namba ya NIDA na kivuli cha nakala ya kitambulisho
chake ambayo kwasasa imesitishwa.
MAMBO
MUHIMU YA KUYAFAHAMU KABLA HUJAOMBA NAMBA YAKO YA NIDA;-
1. Kutambua
majina ya muombaji yaani jinala kwanza na jina la ukoo.
2. Kutambua
tarehe, mwezi na mwaka aliozaliwa muombaji.
3. Kutambua
majina ya mama wamuombaji yaani jina la kwanza na la mwisho la mama wa
muombaji.
4. Kuweza
kutambua na kuandika msimo wa namba za usalama zitakazotolewa na mfumo ili
kuthibitisha kuwa muombaji sio robot.
NB: KUMBUKA KUJAZA NAMBA ZA USALAMA UTAKAZOPEWA NA
MFUMO CHINI YA FOMU YA UJAZAJI KAMA ZILIVO KWA KUANGALIA NAMBA, ALAMA, HERUFI
KUBWA NA NDOGO NA ENDAPO UTAKOSEA BASI REFRESH BROWSER YAKO ILI UWEZE KUPEWA
NAMBA ZINGINE.
Ili uweze kufahamu kikamilifu namba yako ya NIDA kwanza kabisa hakikisha una
kifurushi cha MB na ni lazima ufuate
kiumakini hatua zifuatazo bila kuacha hata kipengele kimoja. Hatua izo ni ;-
1. 1.Ingia
kwenye browser ya computer yako au simu janja , unashauriwa kutumia browser
yenye uzoefu mkubwa ya Google Chrome.
3.Baada ya fomu ya kuomba namba ya NIDA kujitokeza utatakiwa kujaza kama fomu inavyoeleza yaani majina na tarehe ya kuzaliwa na bila kusahau kumalizia na neno lililojizalisha chini ya fomu na mwishoni bonyeza neno Tuma ili kuipata namba yako.
Baada ya kumaliza kujaza kila kitu utaona namba yako
ya NIDA ikijitokeza kwenye box
mstari wa chini kabisa ya page yako ikianzia na mwaka wa kuzaliwa, mwezi wa
kuzaliwa na tarehe, namba ya fomu na namba zingine kukamilisha namba zote
zakitambulisho cha uraia.
Bila shaka utakua umefuata na kufanikiwa kirahisi
kabisa kutambua namba yako ya NIDA
kwa njia ya mtandao. Tafadhali endelea kufuatilia makala yetu kujua mengi
yanayojiri na kujifunza mambo mbalimbali yanayoendelea nchini na duniani kuhusu
elimu na teknolojia pia kumbuka kutuachia maoni yako hapa chini, ahsante.
Comments
Post a Comment